Katika tuzo za wachekeshaji zilizogawiwa leo Februari 22, 2025. Mchekeshaji Dogo Sele ndio amezifungua tuzo hizo za Tanzania Comedy Awards zilizotolewa The Super Dome Masaki kwa kushinda kipengele cha ‘Best Funny Kid’.
Hata hivyo katika tuzo hizo Coy Mzungu ambaye ni mchekeshaji na mwanzilishi wa jukwaa la vichekeso ‘Cheka Tu’ ametunukiwa Tuzo Maalumu ya ‘Game Changer’.
Katika tuzo hiyo Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alimtangaza msConrad Kennedy Coy, ‘Coy Mzungu’, kuwa mshindi wa Tuzo Maalumu ya Game Changer katika tuzo za kwanza za Tanzania Comedy Awards.
Coy amepokea tuzo hiyo kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya vichekesho nchini. Hususani kupitia Cheka Tu ambayo imewapa jukwaa wasanii wengi wa vichekesho.

Hata hivyo Mchekeshaji ‘Jol Master’ ameibuka mshindi wa tuzo ya Mchekeshaji Bora Maalum wa Mwaka katika tuzo hizo za Tuzo za Tanzania Comedy Awards.
Katika kipengele hicho, Jol Master alikuwa akichuana na wachekeshaji wengine walioteuliwa, akiwemo Kipotoshi, Deo Matius na Nalim Noseph.
Jol Master ameshindwa kuhudhuria hafla hiyo kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Aidha, Mchekeshaji maarufu, Lucas Mhavile ‘Joti’ ameibuka mshindi wa tuzo ya Best Legend Peoples Choice of The Year.
Hii ni tuzo ya pili kwa Joti kushinda usiku huu wa tuzo, ambapo ya kwanza alishinda kama Best Comedian Actor of the Year.
Kwenye tuzo yake ya pili alikuwa akichuana na wachekeshaji wakongwe wengine wakiwemo Bambo, Asha Boko, Maufundi, Mukwele, Kigwedu, Senga, Muhogo Mchungu na Brother K.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Lakini pia, nae Mchekeshaji Asma Jamida ameibuka tuzo ya Mchekeshaji Bora wa Kike katika tuzo hizo.
Mchekeshaji mwingine aliyeibuka kidedea kwenye tuzo hizo ni Nanga ambae ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wa kiume wa mwaka.
Tuzo hiyo amekakabidhiwa na Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi hapa The Super Dome Masaki
Tuzo ya Shoo bora ya kwenye Runinga imechukukiwa na Kitim Tim ambapo imeshinda kipengele hiyo, mbele ya Tv shoo zingine ambazo ni Futuhi, original comedy na mbambalive.
Neila Manga ashinda tuzo ya Best Female stand up comedian of the Year
Pia, Neila Manga ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wima wa kike ambapo alikuwa akiwania pamoja na wachekeshaji wengine ambao ni Mambise na mama Mawigi.
Kwaupande wa Mc Eliud, Mr Sukari ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wa wima ‘Best Stand Up Comedy’ kwenye tuzo za Tanzania Comedy Awards zinazo tolewa hapa Super Dome Masaki.
Ameshinda tuzo hiyo ambayo alikuwa anawania pamoja na wachekeshaji wengine akiwemo Leornado, kipotoshi na Deo Rashid.
Mama mchekeshaji nae hakubaki nyuma, Mama Mawingi ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wa kike wa kidijitali.

Lakini pia kipengele hicho hich kwa upande wa wanaume ameshinda TX Dulla ambapo ameshinda tuzo ya mchekeshaji bora wa digitali akiwashinda Steve , Ndaro, Nanga.
Lakini pia Ndaro na Steve mweusi washinda tuzo ya Best Comedy Duo of the Year.
Hii ni tuzo ya ushirikiano kwenye ushekeshaji Wameshinda tuzo hiyo wakiwapiga chini Nanga na Shafii, Zuli Comedy.

Pia, Safina wa mizengwe ameshinda tuzo ya mwigizaji bora wa vichekesho wa kike, kwenye tuzo za wachekeshaji zinazofanyika hapa The Super Dome Masaki Mgeni Rasmi akiwa Rais Samia Suluhu Hassan.