Haya hapa majina walioitwa kwenye usaili wa ajira za Utumishi

Dar es Salaam. Sekretarieti ya Kuajiri Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza rasmi kuitwa kwenye usaili wa ajira kwa mwaka 2025 kwa walioomba nafasi mbalimbali za kazi za Serikali zilizotangazwa kupitia PSRS. Tangazo hili linawahusu waliowasilisha maombi yao hivi karibuni na sasa wamechaguliwa kwa ajili ya usaili. Kwa maelezo ya kina, bofya hapa kupata orodha kamili

Maelezo ya msingi kuhusu usaili

Maeneo ya usaili yameorodheshwa katika tangazo rasmi kwa kila nafasi ya kazi. Pia tarehe za usaili, kwa kila nafasi na taasisi zimebainishwa kwenye tangazo la PSRS. Pia waliotwa wanalazimika kuripoti mapema kama ilivyoagizwa. Soma tangazo lote kwa makini kwani kila nafasi inaweza kuwa na maagizo tofauti ya usaili. Angalia tangazo hapa

Vitu vinavyohitajika

Waliotwa wanalazimika kuleta vyeti halisi, hii ni pamoja na nakala za vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa, na kitambulisho cha taifa (kadi ya NIDA au kitambulisho kingine). Pia barua ya usaili, Nakala ngumu ya barua ya kuitwa kwenye usaili inahitajika.

Pia wanapaswa kufika kwenye eneo la usaili kwa wakati uliobainishwa.  Na kufuata maagizo yote yaliyotolewa kwenye tangazo la usaili kwa makini.

Waliotwa na wakashindwa kuwasilisha vyeti halisi au wanaochelewa kufika wanaweza kuondolewa kwenye mchakato bila kuzingatiwa zaidi.

Fursa hii ya usaili wa 2025 ni hatua muhimu kwa wale wanaotaka kujiunga na utumishi wa umma. Waliotwa wanashauriwa kujiandaa vizuri kwa kufuata maagizo yote, kuleta nyaraka zinazohitajika, na kufika kwa wakati.

Hata hivyo kwa wale waliokosa nafasi hapo awali, fursa ya kuomba tena inapatikana pale nafasi zinapojitokeza. Angalia majina na maelezo zaidi ya usaili, jitayarishe vyema na chukua hatua yako ya kwanza kuelekea kazi ya Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *