Katika kile kinaonekana ni jaribio jingine la kutupilia mbali madai ya Merekani, rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amesema tuhuma kuwa wazungu nchini humo wanalengwa ni za uongo na hazina msingi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa yake ya kila wiki kwa raia wa nchi hiyo, rais Ramaphosa amewataka raia wa nchi hiyo kutokubali kugawanywa na watu kutoka nje na kwamba wanapaswa kukataa kwa nguvu zote nadharia kuwa wazungu nchini humo wanabaguliwa.
Kauli yake anaitoa wakati huu bilionea Elon Musk, akiendeleza madai yake kuwa utawala wa Pretoria unafumbia macho vitendo vya kibaguzi na mashambulio dhidi ya wazungu wachache nchini humo.
Mwezi uliopita Marekani ilitangaza kusitisha msaada wa kifedha kwa nchi hiyo kutokana na kile rais Donald Trump, alisema nchi hiyo inawabagua wazungu huku akitoa nafasi kwa wanaotaka kuondoka kuomba hifadhi Marekani.
Madai ya Marekani yanatokana na matukio ya kulengwa na nyimbo za ukombozi zinazoimlbwa na viongozi wa chama cha upinzani nchini humo EFF, nyimbo zinazoashiria ubaguzi dhidi ya wazungu.