“Hatutajadili mamlaka ya Lebanon”, asema Rais Aoun baada ya Israel kuua Walebanon 15

Rais wa Lebanon, Joseph Aoun amesema “mamalaka ya kujitawala Lebanon na ardhi yake ni jambo lisiloweza kujadiliwa”. Amesema hayo baada ya vikosi vya Israel kuwafyatulia risasi na kuwaua Walebanon waliokuwa wamekimbia makazi yao kusini mwa Lebanon na waliokuwa wakirejea katika miji yao, huku muhula wa mwisho wa kuondoka askari hao makatili ukimalizikka.