Hatua ya Trump kuondoa ufadhili; Wafanyakazi katika mashirika Tanzania wana siutafahamu

Hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kusaini agizo la kuiondoa nchi hiyo katika Shirika la Afya Duniani (WHO) siku chache zilizopita imeanza kuleta athari kadhaa hususan barani Afrika kama ilivyokuwa ikitarajiwa.