Hatimaye moshi mweupe wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) umeonekana jijini Dodoma, baada ya Suleiman Ikomba kutangaz…

Hatimaye moshi mweupe wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) umeonekana jijini Dodoma, baada ya Suleiman Ikomba kutangaz…

Hatimaye moshi mweupe wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) umeonekana jijini Dodoma, baada ya Suleiman Ikomba kutangazwa kuwa Rais mpya wa chama hicho kwa awamu nyingine, akimshinda aliyekuwa Rais, Leah Ulaya, kwa kura 608 dhidi ya 260.

Uchaguzi huo uliodumu tangu Jumatatu, Juni 9, 2025 na kuhitimishwa alfajiri ya leo Juni 10, pia umeweka safu mpya ya uongozi ambapo Joseph Misalaba amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu na Nashon Kidudu akishika nafasi ya mweka hazina.

Ni mwanzo mpya wa uongozi ndani ya CWT, ukilenga kuendeleza maslahi ya walimu nchini.

#azamnewsupdates
✍George Mbara
Mhariri| @official_jennifersumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *