Hata kiongozi wa upinzani Israel amshutumu Netanyahu kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha vita Ghaza

Kiongozi wa upinzani katika utawala wa Kizayuni wa Israel amemshutumu waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano Ghaza na kubadilishana mateka na Hamas baada ya kuchelewesha zoezi la kuwaachia huru Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala huo.