“Hapana” ya watumiaji wa X wa Iran kwa ombi la Trump: Hatutazungumza na Marekani kwa sababu hatuiamini!

Parstoday- Watumiaji wa Kiirani wa mtandao wa kijamii wa “X” wameitaja hatua ya Rais wa Marekani ya kujionyesha kuwa tayari kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni hadaa na udanganyifu mkubwa wa Washington.