Hamas yaukosoa utawala wa Kizayuni kwa kukwamisha utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha mapigano

Kiongozi wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni anaendelea kukwamisha utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha mapigano na kubadilishana kwa uhuru wafungwa na mateka.