Hamas yatoa wito wa maandamano makubwa kupinga mipango ya kuwaondoa Wapalestina huko Gaza

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa wito kwa Wapalestina, Waarabu, Waislamu na watu huru kote duniani kushiriki katika harakati ya kimataifa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, ili kupinga mipango ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuwaondoa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kulikalia kwa mabavu eneo hilo.