
Hamas imetangaza vifo vya mkuu wake wa serikali, Essam al-Dalis, pamoja na Meja Jenerali wake Mahmoud Abu Watfa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Gaza, katika milipuko mashambulizi ya anga ya Israel ambayo tayari yamesababisha vifo vya mamia kadhaa, na kuunja makubaliano ya usitishaji vita ambayo yalifikiwa mwezi Januari.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mkuu wa serikali na waziri wa mambo ya ndani kutoka Hamas wameuawa katika mashambulizi ya Israeli huko Gaza.
Kwa mujibu wa Baraza la Mahusiano ya Kigeni la Ulaya, Essam al-Dalis alizaliwa mwaka wa 1966 na aliishi katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Gaza. Mwalimu wa zamani, aliye kuwa na mke na baba wa watoto sita, alichaguliwa kwenye uongozi wa Hamas huko Gaza mnamo mwezi Machi 2021. Kisha, Juni 2021, akawa mkuu wa utawala wa serikali ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Al-Dalis hapo awali alikuwa mkuu wa chama cha wafanyakazi wa UNRWA huko Gaza. Pia aliwahi kuwa mshauri wa Waziri Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh. Mnamo mwezi Novemba 2023, aliepuka kifo katika shambulio la bomu la Israeli la muundo wa Hamas ambamo alikuwepo na viongozi wengine.
Mahmoud Abu Watfa, mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Hamas, alikuwa msimamizi wa jeshi la polisi la kundi hilo. Alituma tena vikosi vya polisi vinavyohusika na utii wa raia na kudumisha utulivu, kulingana na Ynet News. Alionekana kwenye video mwezi Januari mwaka huu akiahidi kujenga upya Ukanda wa Gaza na utawala wa Hamas.
Vifo viwili muhimu vya Hamas, pamoja na vile vya mkurugenzi mkuu wa huduma za usalama wa ndani, Jenerali Bahjat Abou Sultan, vilivyokumbwa na mashambulizi ya mabomu ya Israel usiku wa Jumatatu 17 kuamkia Jumanne Machi 18. Shirika hilo lilmetangaza, muda mfupi kabla ya saa sita mchana, idadi mpya ya vifo vya watu 413, ikizingatiwa kuwa Marekani inabeba “jukumu kamili” kwa mashambulizi ya Israeli yaliyofanyika jana usiku huko Gaza.