HAMAS yasitisha mchakato wa kuwaachia mateka kutokana na Israel kukiuka makubaliano ya kusitisha vita

Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa, zinasitisha mchakato wa kuwaachia huru mateka wa Israel uliopangwa kutekelezwa Jumamosi ijayo hadi litakapotolewa tangazo jengine, kutokana na utawala wa Kizayuni kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Ghaza.