Hamas yasisitiza: Watu wa Palestina watasalia imara katika ardhi yao

Harakati ya Mpambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imekariri upinzani wake dhidi ya matamshi yaliyotolewa Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu suala la kuwahamusha makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza kwa kisingizio cha kulijenga upya eneo hilo.