Hamas yasifu msimamo wa viongozi wa Afrika dhidi ya Israel

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina , Hamas,  imesifu msimamo wa “kiadilifu na jasiri” wa viongozi wa Afrika kuhusu mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, pamoja na upinzani wao mkali dhidi ya kampeni ya kikatili inayoendelea dhidi ya Wapalestina.