HAMAS yasema imejiandaa ‘kwa chochote kitachotokea’ baada ya ‘onyo la mwisho’ alilotoa Trump

Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kwamba, zimejiandaa kwa “chochote kitachotokea” na zingali ziko kwenye hali ya “tahadhari kamili”, zikisisitiza kuwa, vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel vya kuanzisha tena vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza havitatoa hakikisho kwa utawala huo dhalimu la kuweza kuwakomboa mateka wake.