Hamas yapinga vikali kauli ya Trump, yanasema usitishaji mapigano ndio njia pekee ya kuwarudisha mateka wa Israel

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imelaani wito wa Rais wa Marekani wa kufutwa usitishaji vita katika eneo la Ukanda wa Gaza hadi pale harakati hiyo ya mapambano ya ukombozi wa Palestina itakapowaachia huru mateka wote wa Israel waliosalia katika muda wa siku chache, ikisema Donald Trump lazima akumbuke kwamba njia pekee ya kurejea mateka wa Israel ni kuheshimu mapatano hayo.