Hamas yalaani mashambulizi huku Israel katika Ukingo wa Magharibi

Harakati ya muqawama ya Hamas imelaani uamuzi wa Israel wa kupanua mashambulizi yake ya kijeshi katika Ukingo wa Magharibi wa kaskazini, ikisema kuwa uchokozi huu unaonesha nia hatari ya utawala wa kikoloni wa Israel kuendelea na vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina.