Hamas yakabidhiwa mapendekezo mapya ya Israel kuhusu usitishaji mapigano

Wapatanishi toka nchi ya Qatar na Misri, wamekabidhi mapendekezo mapya ya Israel ya usitishaji wa mapigano huko Gaza kwa kundi la Hamas, mapendekezo ambayo hata hivyo afisa mmoja wa Hamas amesema kuna mambo mawili ambayo hawakubaliani nayo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Punde baada ya kukabidhiwa mapendekezo hayo, kundi la Hamas limesema linayapitia kwa kina kabla ya kutoa msimamo wake ikiwa inayakubali au la, ingawa tayari kundi hilo limeonesha kutoridhishwa na matakwa ya Israel.

Katika mapendekezo haya, kwa mara ya kwanza Israel imejumuisha takwa kwa kundi la Hamas kuweka silaha chini, pendekezo ambalo tangu awali limekuwa likipingwa na Hamas.

Israel imeendelea kutekeleza mashambulio ya anga katika maeneo mbalimbali katika Ukanda wa Gaza.
Israel imeendelea kutekeleza mashambulio ya anga katika maeneo mbalimbali katika Ukanda wa Gaza. REUTERS – Stringer

Watu wa karibu na kundi hilo, wanasema pamoja na kuwa liko tayari kufikia makubaliano na Israel, linadai mpango wowote wa usitishaji mapigano lazima uhusishe wanajeshi wa Israel kuondoka Gaza na kuacha mashambulio yoyote ya uchokozi.

Aidha katika mapendekezo haya, Israel inataka kuachiwa mara moja kwa mateka wote waliosalia chini ya himaya ya kundi hilo na washirika wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *