Hamas yakabidhi ICRC miili minne ya mateka wa Israeli, miili iko nchini Israeli

Hamas imekabidhi, siku ya Alhamisi, Februari 20, kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) majeneza manne yamiili ya mateka wa Israeli huko Gaza, ikiwa ni pamoja na miili ya watoto wawili wa Bibas na mama yao, ambao walikuwa ishara ya ugaidi ulioikumba Israeli wakati wa shambulio la Hamas Oktoba 7, 2023. Miili hiyo imesafieishwa nchini Israeli.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

“Hii itakuwa siku ngumu sana kwa taifa la Israel, siku ya huzuni, siku ya kufadhaisha sana, siku ya maombolezo,” Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema.

Wapiganaji wa Hamas waliojifunika nyuso zao huku wakijihami kwa silaha wakionyesha kwenye jukwaa lililowekwa huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza majeneza manne meusi, kila moja likiwa na picha ya mmoja wa mateka wa Israeli. Juu ya jukwaa, bango linaonyesha Benjamin Netanyahu kama mtu asiye na huruma.

Kisha majeneza hayo yalihamishiwa kwenye gari ndogo (4×4) nyeupe za Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ambayo iliondoka eneo hilo. Karibu, mamia ya watazamaji walitazama tukio hilo wakiwa nyuma ya uzio. Jeshi la Israeli limesema kuwa limepokea miili ya mateka hao.

Msafara uliingia Israeli

Msafara huo ulipitia Kissufim, kusini mwa Israeli, ambapo watu kadhaa walikuwa wamekusanyika na bendera za Israeli au njano – rangi ya mateka – na kwenda hadi Taasisi ya Kitaifa ya Uchunguzi mifupa ya Abu Kabir huko Tel Aviv ambapo, kulingana na jeshi, miili hiyo itapitia “utaratibu wa utambuzi.” Msafara uliokuwa umebeba majeneza hayo ulipita kwenye lango la taasisi hiyo muda mfupi kabla ya saa 7:30 mchana sa za huko.

Miili iliyokabidhiwa kwa mujibu wa Hamas, ni ya Ariel na Kfir Bibas, wenye umri wa miaka 4 na miezi 9 mtawalia siku ya kutekwa nyara, Oktoba 7, 2023, pamoja na ya mama yao, Shiri Bibas na Oded Lifshitz, mwenye umri wa miaka 83 siku hiyo. Walirejeshwa kwa kubadilishana na kuachiliwa kwa Wafungwa wa Kipalestina, zoezii lililopangwa siku ya Jumamosi, kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Usitiswaji mapigano ulianza kutumika Januari 19, baada ya miezi 15 ya vita vikali huko Gaza vilivyochochewa na shambulio la Hamas katika ardhi ya Israeli.

Tangu kuanza kwa usitishaji mapigano uliosimamiwa na Qatar, Misri na Marekani, mateka 19 wa Israeli wameachiliwa, badala ya Wapalestina zaidi ya 1,100 waliokuwa wakishikiliwa na Israeli wakati wa awamu ya kwanza ya mapatano hayo. Serikali ya Israeli siku ya Alhamisi, Februari 20, imeshutumu Hamas kwa kudumisha “ibada ya kifo.” “Hamas sio vuguvugu la upinzani, Hamas (inaendelea) ibada ya mauaji, inaua, kutesa na kuandamana na maiti,” msemaji wa serikali David Mencer amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Hatua ya kurejeshwa kwa miili ya mateka wanne wa Israeli kutoka Hamas hadi Gaza ni “ya kinyama na ya kikatili”, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu amesema.

 “Kwa mwendo mmoja”

Hii ni mara ya kwanza kwa Hamas kukabidhi miili ya mateka waliofariki. Jumamosi, Februari 22, Hamas itawaachilia huru mateka sita wakiwa hai. Makubaliano hayo yanatoa nafasi ya kuachiliwa huru kwa jumla ya mateka 33, wakiwemo wanane waliofariki dunia, ifikapo mwisho wa awamu yake ya kwanza Machi 1, na hivyo Israeli kuachilia huru Wapalestina 1,900 wanaoshikiliwa na Israeli.