Hamas ‘yajiweka sawa’ baada ya Israel kufanya shambulio la kinyama Jenin

Wanajeshi wa Israel wamewauwa shahidi Wapalestina kumi na kuwajeruhi wengine 35 katika shambulio dhidi ya mji unaokaliwa kwa mabavu wa Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kupelekea Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kutoa wito kwa vijana wa Kipalestina kujikusanya na kujiandaa kujibu uchokozi huo wa vikosi vamizi vya Wazayuni.