HAMAS waitunishia misuli Israel kwa kutokeza hadharani na bunduki zake walizoteka Oktoba 7, 2023

Katika hatua inayoonekana kuwa ya kuonyesha uwezo wao wa kijeshi na kuutunishia misuli utawala wa Kizayuni wa Israel, wanamapambano wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, jana walijitokeza na bunduki za Israel aina ya Tavor wakati wa makabidhiano ya wanajeshi wanne wa kike wa utawala huo wa Kizayuni katika mji wa Ghaza.