Hamas: Ukingo wa Magharibi utakuwa uwanja ujao wa vita kati ya Israel na muqawama

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa inaamini kuwa eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na Israel litakuwa uwanja ujao wa makabiliano makubwa kati ya utawala wa Israel na muqawama wa Palestina.