Hamas: Tangazo la Marekani la kuwaondoa wakazi wa Gaza ni ushirikiano katika uhalifu

Sami Abu Zuhri, kiongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), amesema kuwa tangazo la mara kwa mara la Marekani la kuwatimua wakazi wa Ukanda wa Gaza katika eneo hilo kwa kisingizio cha kulijenga upya ni kielelezo cha kushiriki Washington katika jinai za utawala uo, baada ya Israel kufanya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miezi 15.