Hamas: Makubaliano ya kusitisha vita ni matunda na Muqawama wa miezi 15 wa wananchi wa Ghaza

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kuwa, kulazimika utawala wa Kizayuni kukubali kusimamisha vita na kukomesha mauaji yake ya kimbari dhidi ya wananchi wa Ghaza, ni matunda ya Muqawama na kusimama imara wananchi wa ukanda huo kwa zaidi ya miezi 15.