HAMAS: Kuwa na silaha ni haki ya kisheria ya Muqawama na kuachana nazo ni jambo lisilowezekana

Hazem Qassem, msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ameashiria matamshi yaliyonasibishwa na kiongozi mwandamizi wa harakati hiyo Musa Abu Marzouk na kusisitiza kwamba: “Hamas inaendelea kutumia silaha za Muqawama kama haki halali na ya kisheria na haitalegeza msimamo juu ya suala hilo”.