
Hamas imetangaza siku ya Jumanne, Februari 18, kwamba mateka sita wa Israeli walioshikiliwa katika Ukanda wa Gaza wataachiliwa huru siku ya Jumamosi, Februari 22. Kabla ya hapo, siku ya Alhamisi, Februari 20, kundi hili litarejesha miili minne ya mateka kwa taifa la Israeli. Wakati majina ya mateka walio hai yametolewa, yale ya mateka waliofariki bado hayajathibitishwa.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Hii ni mara ya kwanza tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas kuanza Januari 19 kwa miili ya mateka kurejeshwa. Serikali ya Israeli imethibitisha kwamba itakabidhiwa miili minne ya mateka siku ya Alhamisi, Februari 20, lakini bila kutoa maelezo zaidi, anaelezea mwandishi maalum wa RFI huko Jerusalem, Pierre Olivier. Hapo awali Hamas iliripoti kuwa Shiri Bibas na watoto wake Kfir na Ariel ni miongoni mwa maiti nne. Familia ya Bibas imekuwa ishara ya mkasa wa mateka wa Israeli waliotekwa Oktoba 7, 2023 wakati wa shambulio ambalo halijawahi kufanywa na Hamas.
Wakati baba, Yarden Bibas, aliachiliwa mnamo Februari 1, hatima ya mkewe Shiri na wavulana wao bado haijulikani. Nchini Israeli, hakuna tumaini la kuwaona wakiwa hai tena, lakini kwa kukosekana kwa uthibitisho, familia inabaki kuwa angalifu. “Tulishtushwa na tangazo la […] Hamas la mpango wa kurudishwa kwa wapendwa wetu Shiri, Ariel na Kfir siku ya Alhamisi. (…) Tunasema wazi kwamba, ingawa tunafahamu habari hii, bado hatujapata uthibitisho wowote juu ya suala hili,” famili imesema, na kuongeza kuwa “mpaka tupate uthibitisho usioweza kukanushwa, pambano letu litaendelea.”
Israel inaandaa kurejea kwa miili hii ya kwanza tangu Januari 15. Mabaki yatahamishiwa katika taasisi ya Tiba ya Uchunguzi huko ya Tel Aviv baada ya kupokelewa. Mara tu vitambulisho vitakapofanywa ndipo majina yatawasilishwa kwa familia.
Awamu ya pili ya mazungumzo ya kusitisha mapigano kuanza hivi karibuni
Jumamosi, Februari 22, mazungumzo kati ya Israeli na Hamas yatarejelewa. Hamas itawaachilia mateka sita wakiwa hai. Muungano ya familia za mateka wametanagaza majina yao: Eliya Cohen, Tal Shoham, Omer Shem Tov, Omer Wenkert, Hicham al-Sayed na Avera Mengistu. Mpatanishi mkuu wa Hamas Khalil al-Haya amesema kuwa Israeli itaachilia idadi maalum ya wafungwa wa Kipalestina kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Jumla ya mateka 33 wa Israeli wanatazamiwa kuachiliwa wakati wa awamu ya kwanza ya usitishaji vita, ambao inakamilika Machi 1, badala ya wafungwa 1,900 wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israeli; Miili mingine minne ya mateka litakabidhiwa baada ya marejesho yaliyopangwa kufanyika Februari 20. Tangu kuanza kwa usitishwaji mapigao huo, na kabla ya mabadilishano yaliyopangwa kufanyika Februari 22, mateka 19 wa Israeli na wafungwa 1,134 wa Kipalestina wameachiliwa huru. Kufikia Februari 18, watu 70 bado wanazuiliwa huko Gaza, takriban 35 kati yao wamekufa, kulingana na jeshi la Israeli.
Wakati awamu ya kwanza ya usitishaji vita inakamilika Machi 1, mazungumzo ya awamu ya pili yanatarajiwa kuanza “wiki hii,” kulingana na Gideon Saar, Waziri wa Mambo ya Jje wa Israeli. Israel anadai, kwa maneno yake, “kuondolewa kabisa kwa wanajeshi katika Ukanda wa Gaza.” Awamu hii ya pili inatakiwa kuachiliwa kwa mateka wote na mwisho wa vita. Lakini mustakabali wa Gaza haujulikani sana, kati ya matamanio ya Marekani ya Donald Trump, yanayoungwa mkono na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, na msimamo wa nchi za Kiarabu; nchi hizi zinapinga vikali mpango wa Washington wa kuiweka Gaza chini ya udhibiti wa Marekani na kuwafukuza wakazi wake milioni 2.4.