HAMAS, Jihadul-Islami, Wabunge wa US wapinga na kulaani matamshi ya Trump ya kuipora Ghaza

Matamshi ya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba nchi hiyo itawahamisha Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza na kulitwaa na kulimiliki eneo hilo la Palestina yamelaaniwa na kukosolewa vikali ndani na nje ya Marekani.