HAMAS iko tayari kuwaachia mateka wote mkabala wa Israel kuondoka kikamilfu Ghaza na vita kuhitimishwa

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS Hamas imependekeza kubadilishana mateka wote wa Israel kwa mateka Wapalestina “kwa mpigo” wakati wa awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano Ghaza, kwa lengo la kufikia mapatano ya kudumu na jeshi la utawala wa Kizayuni kuondoka kikamilifu katika eneo hilo.