Hamas: Hatua ya Pili ya Usitishaji Mapigano Gaza ni njia pekee ya kuachiliwa mateka wa Israel

Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas,  ameulaumu utawala haramu wa Israel kwa kutaka kurejesha uvamizi wake dhidi ya Gaza na kukwepa makubaliano ya usitishaji mapigano, akisisitiza kuwa njia pekee ya kuhakikisha kuachiliwa kwa mateka wa Israel ni kuanza hatua ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano.