HAMAS: Hadi sasa hakuna makubaliano yoyote kuhusu awamu ya pili ya mazungumzo ya Ghaza

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa, mazungumzo baina yake na utawala wa Kizayauni wa Israel yamesimama na hakuna maendeleo yoyote ya maana kuhusu awamu ya pili ya mazungumzo ya kusimamisha vita huko Ghaza.