Haki na wajibu wa watoto kwa mama yao

Neno mama limetajwa katika Qur’an mara 28 kwa tamko la umoja na wingi. Kawaida, neno hili linapotajwa katika Qur’an hutangamana na msamiati unaoelezea hali halisi ya umama, iwe ya kibiolojia au ya kihisia.

Kwa ujumla, Qur’an Tukufu imeeleza kwa kina kuhusu sifa ya umama, ikifafanua vipengele vyake vya kimaumbile na vya kiroho, ikabainisha haki anazostahiki mama na wajibu anaoubeba.

Kwa mtazamo wa Qur’an, umama ni hadhi ya heshima, huruma, kujitolea na ibada, inayomletea mwanamke daraja la juu mbele ya Muumba wake na mbele ya jamii..

Neno mama limetajwa katika Qur’an mara 28 kwa tamko la umoja na wingi. Kawaida, neno hili linapotajwa katika Qur’an hutangamana na msamiati unaoelezea hali halisi ya umama, iwe ya kibiolojia au ya kihisia.

Misamiati  inayohusina na umama

Ujauzito: Miongoni mwa msamiati unaotumika kumwelezea mama ni ujauzito, ambayo huashiria jukumu la uzazi la mama. Qur’an inaeleza kwa uwazi mateso ya kimwili na kiakili anayopitia mwanamke katika kipindi cha ujauzito:

Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu..” (Quran 46: 15)

Aidha, Allah Mtukufu anaashiria kuwa ujauzito ni miongoni mwa siri za uwezo wake, na hakuna binadamu yeyote mwenye mamlaka juu ya jambo hilo: “Na hakuna mwanamke anayebeba mimba wala anayezaa isipokuwa kwa ujuzi Wake.” (35: 11)

Tumbo la mama: Neno hili linatajwa kwa muktadha wa kuonyesha uumbaji wa mwanadamu katika hatua za tumboni. Kama kauli yake Allah Mtukufu: “Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu uumbaji baada ya uumbaji.”
(39: 6) .

Kunyonyesha na kuachisha: Kunyonyesha ni dhana iliyo karibu mno na  sifa ya umama, na Qur’an huitaja kuelezea umuhimu wa mama wa kimalezi na hata athari zake za kisharia.

Mfano kauli yake Allah: “Na mama zenu waliowanyonyesha.”
(4: 23) Kadhalika kauli yake“Na tukamfunulia mama wa Mūsā: Mnyonyeshe.”(28: 7) Baada ya kunyonyesha hufuata kuachishwa kwake (fṭām), na Qur’an imetaja: “Na kuachishwa kunyonya kwake ni ndani ya miaka miwili.” (31: 14) Hii inaonyesha hatua ya kuhitimisha mchakato wa malezi ya awali ya mtoto.

Qur’an haikuishia kueleza sfa ya umama kwa sura ya kibiolojia tu, bali pia imetaja umama wa kihisia katika aya nyingi. Mfano wa hofu aliykuwa nayo mama yake Nabii Musa.

“Basi ukihofia usalama wake, mtie katika mto.”(28: 7) Hili linaonyesha hisia ya hofu ya mama kwa ajili ya mwanawe – jambo la msingi katika dhima ya umama. Aya nyingine:“Mama asidhuriwe kwa sababu ya mtoto wake.”
(2: 233) Wanazuoni walieleza: maana ni kuwa mwanamume haruhusiwi kumnyang’anya mama mtoto wake ili amkabidhi mwanamke mwingine.

Haki na wajibu wa mama

Umama huweka haki na majukumu juu ya mwanamke. Qur’an imeeleza baadhi ya haki zake, kama vile: Qur’an Tukufu imeweka haki muhimu kwa mama, na imehimiza kuzitekeleza bila masharti, zikiwemo:

Kufanyiwa wema: Allah Mtukufu ameamuru watu wawafanyie wema wazazi wao, na amri hii haina masharti – hata ikiwa wazazi ni makafiri au wapagani. Amesema: Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat’ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani,.”(31: 15)

Aidha, Qur’an imetanguliza wema kwa mama kabla ya baba, kutokana na taabu alizokutana nazo katika kubeba mimba na kulea. Amesema: “Na tumemuusia mwanadamu awafanyie wema wazazi wake; mama yake amembeba kwa taabu na akamzaa kwa taabu. Na kubeba kwake na kumwachisha kunyonya ni miezi thelathini.”
(46: 15)

Kusema nao kwa adabu: Mtu anatakiwa azungumze na wazazi wake kwa heshima na kwa maneno mazuri, bila ukali wala kinyongo. Amesema: “Na waambie maneno ya heshima.”
(17: 23). Hili pia ni onyo dhidi ya ukimya unaoumiza au maneno ya chuki dhi ya wazazi – mtoto anatakiwa awe mwepesi wa kuwasikiliza wazazi wake, kuwanao karibu asiwatenge, na kuwatendea wema kwa maneno.

Unyenyekevu na kuwaombea dua: Hili linaeleza adabu ya vitendo, yaani namna mtoto anavyowahudumia wazazi wake kwa huruma, unyenyekevu, na ukaribu. Qur’an inafananisha hali hiyo kwa kusema: Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.  (17: 24)

Wajibu wa mama ulioelezwa katika Qur’an

Kunyonyesha.: Hili ni jukumu la kwanza kabisa kwa mama, kama alivyoamrisha Allah: “Na mama wanyonyeshe watoto wao kwa miaka miwili kamili.”(Al-Baqarah: 233).Qur’an imeeleza kwa kina hukumu mbalimbali kuhusu kunyonyesha, ikionyesha umuhimu wake katika makuzi ya mtoto na maendeleo ya afya na akili yake.

Malezi (Tarbiya):  Hili ndilo jukumu kuu zaidi kwa mama. Huenda shughuli ya kunyonyesha mtoto kunyonya ikafanywa na mtu mwingine, lakini kazi ya malezi haiwezi kufanywa na yeyote ila mama. Qur’an imeashiria umuhimu kupitia malezi ya Luqmān kwa mwanawe: “Ee mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu; hakika ushirikina ni dhulma kubwa.”
(31: 13)

Malezi ya kweli huanza kwa kumjenga mtoto katika msingi wa imani, kumfundisha maadili na kumkuza kuwa mtu mwema wa dunia na akhera.

Mwandishi anapatikana kwa simu 0712 690 811

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *