Haiti: Afisa wa Polisi wa Kenya atoweka baada ya kutokea shambulio

Afisa wa polisi kutoka nchini Kenya ambaye ni sehemu ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti hajulikani alipo baada ya kutokea kwa shambulio ambalo lilitekelezwa na watu silaha

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Taifa hilo la Afrika Mashariki linaoongoza ujumbe wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa, kikosi ambacho kinalenga kuwasaidia polisi wa Haiti kupambana na makundi ya watu wenye silaha wanaokalia sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Licha ya kutumwa kwa polisi hao, Haiti imeedelea kukabiliwa na utovu wa usalama unaotekelezwa na makundi ya watu wenye silaha.

Afisa huyo wa Kenya alitoweka siku ya Jumanne ya wiki hii wakati wa harakati za kuliondoa gari la kivita la polisi wa Haiti ambalo lilikuwa limekwama kwenye mtaro unaoshukiwa kwamba ulilimwa kimakusudi na watu hao wenye silaha.

Kenya inaoongoza kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti
Kenya inaoongoza kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti © Odelyn Joseph / AP

Tukio hilo limejiri baada ya afisa mwengine wa Kenya kufariki kutokana na majeraha ya risasi wakati wa oparesheni ya siku ya Ijumaa.

Ujumbe wa Kenya umekuwa ukikabiliwa na ukosoaji kutoka nyumbani na hata kukabiliwa na changamoto za kisheria.

Nairobi imewatuma karibia polisi wake 700-katika oparesheni hiyo yenye walinda usalama Elfu Moja kulingana na takwimu za AFP.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *