#HABARI:Timu ya Taifa ya Riadha ya Tanzania (Marathon) yenye wakimbiaji wanne imeondoka alfajiri ya leo kuelekea mjini Paris, nchini Ufaransa tayari kwa mashindano ya Olympic ambapo wakimbiaji wetu Alphonce Simbu, Gabriel Geay, Magdalena Shauri na Jackline Sakilu wataanza kampeni ya kusaka medali tarehe 10-11 mwezi wa nane 08, 2024.