#HABARI:Serikali imeshauriwa kuanzisha Klabu za masuala ya fedha katika shule mbalimbali hapa nchini, ili wanafunzi wafundishwe matumizi ya fedha, umuhimu wa kujiwekea akiba tangu wakiwa wadogo lakini pia kupata mabalozi wazuri wa masuala ya fedha.
Ushauri huo umetolewa na Mlezi wa Klabu, katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Liwale, Mwalimu Mustafa Ahmadi Likambako, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha.
Naye Afisa Mchambuzi Hesabu Mwandamizi, kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Bi. Mariam Omari Mtunguja, alisema kuwa wametoa elimu ya masuala ya fedha kwa makundi mbalimbali wakiwepo wanafunzi, wakufunzi, vikundi vya wajasiriamali na wafanyabiashara.