#HABARI:Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe Dkt. Doto Biteko amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutumia fursa ya uwepo wa umeme wa kutosha katika kipindi hiki kufanya matengenezo ya mashine mbalimbali, ambazo hazikuweza kufanyiwa matengenezo kipindi ambacho nchi ilikuwa haina umeme wa kutosha.
Dkt. Biteko ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya umeme vya Ubungo I, Ubungo II, Ubungo III pamoja na kituo cha kudhiti mifumo ya umeme wa gridi yaani Grid control Centre.
https://www.itv.co.tz/news/bitekotanesco-tumieni-umeme-uliopo-kufanya-matengen
(Feed generated with FetchRSS)