#HABARI:Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimependekeza serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kurekebi…

#HABARI:Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimependekeza serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kurekebisha mamlaka ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji katika Muswada wa mabadiliko ya sheria namba 2, 2024 ambao baadhi ya vifungu vyake vinalenga kuanzisha hadhi maalum ya uraia, ili kupunguza mamlaka makubwa aliyopewa katika kutoa na kubatilisha hadhi maalum.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt.Anna Henga Jijini Dar es Salaam.

Mapendekezo ya LHRC.

1. Serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kurekebisha mamlaka ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji ili kuzuia uwezekano wa kusitisha ‘Hadhi Maalum’ pale itakapokuwa imetolewa.

2. Kuondoa mamlaka ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kufanya maamuzi kwa utashi (Discretionary Powers), Mahakama iwe chombo cha mwisho cha utoaji haki.

3. Kupunguza mamlaka makubwa aliyopewa Kamishna wa Uhamiaji katika kutoa na kubatilisha hadhi maalum.

4. Kuweka utaratibu wa kisheria na haki ya kusikilizwa pale kuna nia ya kubatilisha hadhi maalum na jukumu hili, liwe chini ya Mahakama.

5. Kuweka vigezo sawa vya utoaji wa ‘Hadhi Maalum’, ili kutoleta dhana ya ubaguzi kwa makundi au watu fulani.

6. Kufuta kifungu chote cha 37 kama ilivyoamuliwa na Mahakama Kuu katika ya kesi Prisca Chogero dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Na.17 ya mwaka 2023.

7. Kufuta matumizi ya vigezo vya maadili mema, utii na utovu wa maadili kama vigezo vya kutoa ‘Hadhi Maalum’.

8. Tanzanite Card isiwe na ukomo. Uasili wa Tanzania wa diaspora usipokwe.

9. Sharti la kumiliki kampuni kwa kuwa na minority Tanzanian Citizen Stakeholders, liondolewe kwani linapunguza maana ya Hadhi Maalum kwa wenye asili na Tanzania.

10. Diaspora awe na haki sawa za kumiliki ardhi sawa na raia mwingine yeyote wa Tanzania, Diaspora ana uasili sawa sawa na wenyeji.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania