#HABARI:Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Chacha, amesema
Huduma ya Msaada wa Kisheria bure, inayotolewa na Serikali kupitia Kampeni ya Mama Samia legal Aid, imeshafika kwenye mikoa 7 ya awali nchini kusikiliza na kutatua changamoto zinazokabili wananchi na maeneo yenye kuguswa na msaada huo ikionekana migogoro ya Ardhi na Mirathi.
Bw.Eliakim amesema huduma ya Msaada wa Kisheria ni Kubwa na ili kuwafikia Watanzania wengi Wizara inapambana kuhakikisha inafika mikoa 26 ya Tanzania Bara na Mitano ya Zanzibar.
Bwana Eliakim amesisitiza kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa nafasi hiyo ya kutolewa msaada wa kisheria bila malipo kwa Watanzania.