#HABARI: Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mwanza na Shinyanga,litafanyika kwa siku saba kuanzia ta…

#HABARI: Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mwanza na Shinyanga,litafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 21 hadi 27 Agosti, 2024 ambapo jumla ya wapiga kura wapya 400,082 wanatarajiwa kuandikishwa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele,mkoani Mwanza kwenye Mkutano wa Tume na wadau.

“Kwa mkoa wa Shinyanga Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 209,951. Hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 ya wapiga kura 995,918 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,amesema Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima Ramadhani.