#HABARI: Zaidi ya matrekta 500 na power tiller 800 zitazinduliwa wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 iki…

#HABARI: Zaidi ya matrekta 500 na power tiller 800 zitazinduliwa wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 ikiwa ni sehemu ya matrekta 10,000 yanayotarajiwa kununuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema hayo wakati wa Hafla ya Ufunguzi wa Maonesho hayo ya Nane Nane 2024 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma, katika Viwanja vya Nzuguni ambapo amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kufikia matrekta 10,000 ifikapo mwaka 2030.