#HABARI: Wilaya ya Kiteto ni miongoni mwa Wilaya zenye uhitaji mkubwa wa huduma za Msaada wa Kisheria, kutokana na uwepo wa mlolongo wa changamoto za migogoro ya matumizi ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Remidius Mwema, alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria, lililopo katika Viwanja vya Nanenane – Nzuguni Jijini Dodoma ambapo huduma za Msaada wa kisheria zinatolewa bure kwa Wananchi kupitia Kampeni ya Mama Samia legal Aid.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania