#HABARI: Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt.Selemani Jafo, amesema kuzinduliwa kwa sera mpya ya taifa ya biashara kutasaidia kuk…

#HABARI: Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt.Selemani Jafo, amesema kuzinduliwa kwa sera mpya ya taifa ya biashara kutasaidia kukuza uchumi wa nchi, ili kuendana na mabadiliko yaliyotokea ya Kikanda ya Kimataifa, pamoja na kuboresha mazingira ya Biashara, kuongeza ukuaji wa uchumi na kuboresha ustawi wa wananchi.

Dkt.Jafo ameeleza hayo Jijini Dar es Salaam, wakati akiongea na vyombo vya habari katika kuelekea uzinduzi huo utakaofanyika 30 Julai 2024, huku akibainisha kuwa kupitia utekelezaji wa sera ya Taifa ya Biashara ya Mwaka 2023, serikali imefanikiwa kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya biashara baina ya nchi na nchi, Kikanda na Kimataifa kwa lengo la kuongeza fursa za biashara ya bidhaa na huduma kutoka Tanzania.

Sera mpya ya Taifa ya Biashara ina kauli mbiu isemayo, Ushindani wa Bishara katika Kuchochea Kasi ya Mabadiliko ya Kijamii na Uchumi yanayoongozwa na Viwanda.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania