#HABARI: Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso, ameipongeza Kampuni ya AL FRADAWS Investment Company Limited, kutoka Jordan ambayo ni wawekezaji katika uzalishaji wa Mbegu mbalimbali Mkoani Singida kwa Kuja na Suluhisho katika Upatikanaji Maji Mkoani humo Kupitia Teknolojia ya Pivot irrigation System.
Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa yenye changamoto ya vyanzo vya Maji vya uhakika na upatikanaji maji chini ya ardhi.
Akizungumza wakati alipotembelea Kampuni iliyopo Kijiji cha Choda wilayani Ikungi, Waziri Aweso Amesema Teknolojia ambayo inatumiwa na Kampuni ya FRODAWS ni nzuri kwa kuwa inatoa majibu ya uhakika katika Utambuzi wa maeneo yenye maji kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji.