#HABARI: Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema Serikali itawachukulia hatua kali wanasheria vishoka, ambao huwadanganya wananchi juu ya masuala ya kisheria na hivyo kusababisha migogoro katika jamii.
Amesema sasa hivi Serikali imeweka kipaumbele cha msaada wa kisheria, kwenye maeneo ya wakulima na wafugaji, ili kupunguza migogoro ya ardhi na migogoro mingine kwenye jamii.
Ameeleza hayo kwenye banda la Wizara ya Katiba na Sheria, lililopo kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma, ambapo Wananchi wanapatiwa huduma ya msaada wa kisheria bure kupitia Kampeni ya Mama Samia Legal Aid.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania