#HABARI: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Deogratius Ndejembi, ameitaka Menejimenti na watumishi wa Wizara ya …

#HABARI: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Deogratius Ndejembi, ameitaka Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Ardhi kuondoa urasimu na kutoa hati milki za ardhi kwa wakati.

“Tuondoe urasimu, kama mtu ana nyaraka zote zinazohitajika, tuwape hati zao na tukumbuke sisi ni watoa huduma kwa wananchi n ani wizara wezeshi, hati zitolewe kwa wakati na hati zilizotayari wananchi wajulishwe waje wachukue hati zao” amesema Mhe. Ndejembi.

Mhe.Ndejembi amesema hayo wakati wa kikao na wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.