#HABARI: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya Nane Nane 2024 yanayofanyika Kitaifa jijini Dodoma.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, wakati akikagua uwanja wa Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024, na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika Maonesho hayo katika Kanda zote ,ili kuweza kujifunza teknolojia mbalimbali zitazowanufaisha wakulima na wazalisha wa bidhaa za kilimo.
Kauli mbiu ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane 2024 ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.