#HABARI: Watu wanne wakazi wa mkoani Mwanza, wanashikiliwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa kuhusika na tukio la …

#HABARI: Watu wanne wakazi wa mkoani Mwanza, wanashikiliwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa kuhusika na tukio la kurusha Fedha chini sakafuni, wakati wakitoa zawadi jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbroad Mutafungwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari.