#HABARI: Watu nane wa Familia moja katika Mtaa wa Airport, Kata ya Iyela, jijini Mbeya, wamenusurika kifo, baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuwaka moto majira ya saa tano usiku, huku chanzo chake kikiwa bado hakijafahamika.
Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dr Tulia Ackson, amefika katika kata hiyo na kupata taarifa ya tukio hilo.