#HABARI: Wananchi waliopatiwa matibabu ya Macho bure, wilayani Nachingwea mkoani Lindi, wamewaomba wadau wa afya wanaotoa huduma hizo hapa nchini kuongeza muda, kwani uhitaji wa matibabu bado ni mkubwa ukilinganishwa na muda wanaofanya kazi, kwa sababu baadhi ya wagonjwa wanatoka Vijiji vya mbali na kukuta zoezi hilo muda wake umeisha.