#HABARI: Walimu wa Shule ya Sekondari Ivumwe, inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi, iliyopo Kata ya Mwakibete, Jijini Mbeya, wamefunga geti kwa kutumia gogo wakimzuia Mkuu wa Shule hiyo kuingia ndani mpaka pale watakapolipwa stahiki zao.
Wakizungumza na ITV walimu hao wamesema mgomo huo ni endelevu mpaka pale watakapolipwa stahiki zao ikiwemo mishahara na malimbikizo ya posho. ITV inaendelea kumtafta Mkuu wa Shule hiyo pamoja na uongozi wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mbeya, kwa ajili ya ufafanuzi Zaidi.
Hata hivyo wakati walimu wakimsubiri Mkuu wa Shule, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kufanya mazungumzo na walimu.