#HABARI: Wakulima wa zao la Kahawa, mkoani Kagera, wameanza kupanua mashamba yao ya Kahawa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa z…

#HABARI: Wakulima wa zao la Kahawa, mkoani Kagera, wameanza kupanua mashamba yao ya Kahawa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kuendelea kunufaika na bei ya minada ya kahawa iliyopo sokoni.

Wakulima hao wamesema kwa sasa bei ya kahawa imeimarika, ukilinganisha na miaka ya nyuma hali inayowapa hamasa ya kuendelea kupanua mashamba yao ili kunufaika na minada ya kahawa inayoendelea mkoani humo.